.Kutolewa vyeti maalum
..wadau kukata keki ya pamoja
..Slim kutumbuiza
Na Andrew Chale
KILELE
cha Miaka 10 na ‘After Party’ ya onesho la mavazi la ‘Lady in Red
Super Brand’ kinatarajia kufikia tamati usiku wa Jumamosi, Februari 22,
ndani ya Ukumbi ulio na mgahawa wa kisasa wa hadhi jijini Dar es
Salaam, wa Nyumbani Lounge, huku kukitarajiwa kuwa na surprise mbali
mbali kwa wadau watakaojitokeza.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin, wandaaji
wa Lady in red, kila mwaka hapa nchini, alisema, ‘after party’ hiyo ni
maalum kwa ajili ya kutoa shukrani na vyeti maalum kwa wadau
wanaoliunga mkono jukwaa la Lady in red kwa kipindi chote hadi kufikia
hapo ambapo pia watapata wasaha wa kukata keki ya ukumbusho.
“After
party ya miaka 10 ya Lady in red, kwa mwaka huu itakuwa ya aina yake
sambamba na surprise, hivyo nyote munakaribishwa na hakuna kiingilio na
kwa watakaokuwa tayari kujiunga siku maalum pale Nyumbani Lounge,
wafike katika duka la Fabak Fashion, lililopo jirani na kituo cha
Msasani, Kwa Mwalimu Nyerere au kwa kupiga simu namba 0713263363 ama0784263363” alisema Asia Idarous.
Na kuongeza kuwa, pia tiketi maalum za bure zitatolewa mlangoni Nyumbani Lounge, kwa wadau watakaofika. Aidha, alisema msanii wa muziki wa kizazi kipya, Slim Guapo Sosa anayetamba na kibao cha ‘ LOVE YOU ’ na vingine vingi anatarajiwa kuwakonga nyoyo watakaojitokeza kwenye ‘after party’ hiyo.
Party hiyo imedhaminiwa na wadhamini mbali mbali wakiwemo Times fm, Michuzi media group, mo blog, Nyumbani Lounge, Darling air, G one Media na wengine wengi
No comments:
Post a Comment