Pages

Wednesday, February 5, 2014

[BasketBall] : B’Ball Kitaa Chini Ya Mataa, Ijumaa Hii (Februari 7)

IMG-20140203-WA019


Ni Ijumaa nyingine ambayo wajanja wote wa mjini hukutana pale chini ya mataa, viwanja vya Gymkhana ambapo huchezwa mechi mbalimbali za mpira wa kikapu…Kam ilivyo ada, B’Ball kitaa hufanyika mara moja kwa kila mwezi ambapo ilifungua mwaka na mchezo uliopigwa Januari 10 kati ya chuo cha CBE na UDSM, ambapo CBE waliibuka kidedea kwa ushindi mnono. Februari hii, kitawaka tena ambapo timu mbalimbali zitachuana vilivyo.
BBALL1
Huduma ya chakula na vinywaji itakuwepo wakati mechi zikiwa zinaendelea, pamoja na burudani nzuri ya mziki toka kwa Dj PAQ. Kuanzia mida ya saa 1 jioni, jisogeze viwanja vya Gymkhana kuweza kuangalia mechi kali na nzuri zikichezwa Live.
BBALL2
Kiingilio ni BUREEE ! Miguu yako tu kuweza kufika pale na kufurahia burudani nzurii

No comments:

Post a Comment