MSANII maarufu wa muziki wa kikazi kimpya Dully
Sykes juzi aliwaduwaza wapenzi wa muziki wa dansi baada ya kupanda
katika jukwaa la Malaika Bend na kuimba wimbo wa bend hiyo pamoja na
kupiga kwa ufasaha baadhi ya vifaa vya muziki jambo lililowashangaza
wengi na kujikuta akiwainua wapenzi wa muziki vitini na kuanza
kumshangilia.
Tukio hilo lilitokea ndani ya ukumbi wa Dar West uliopo Tabata Jijini
Dar es Salaam ambapo bend ya Malaika ilikuwa ikifanya onesho lake
katika ukumbi huo. Dully alipanda jukwaani baada ya kiongozi wa Malaika
Bend Christian Bella alipomkaribisha jukwaani kuwasalimu wapenzi wake
ambao wengi walikuwa wakitokea maeneo ya Tabata ambapo ni eneo pia
analotoka msanii huyo wa kizazi kimpya.
“…Naomba nimkaribishe Dully apande jukwaani kuwasalimu wanaTabata
ambao ni majirani zake, Dully anakaa Tabata tangu siku nyingi sana mi
nimeingia Tanzania nimemkuta Dully yupo Tabata hadi leo hii anakaa
Tabata,” alisikika Bella akisema mara baada ya Bend yake kupiga nyimbo
kadhaa.
Dully alipanda jukwaani na kuanza kuimba moja ya nyimbo za Malaika
Bend pamoja na kupigiwa vifaa jambo ambalo liliwanyanyua wapenzi wengi
kwenye viti ambao hawakutegemea msanii huyo kumudu miondoko ya bolingo
tofauti na miondoko yake. Baada ya kuimba wimbo mmoja aliomba apewe
gitaa ambalo pia alilicharaza kisawasawa mithili ya mtaalamu na
kushangiliwa.
“…Naomba nimalizie kwa kupiga ‘dram’ ili niwaoneshe wapenzi wangu
mimi ninamudu kupiga vifaa mbalimbali,” alisema Dully. Baada ya kuachiwa
tena dram alipiga kwa ufasaha hivyo kushangiliwa na wapenzi anuai ndani
ya ukumbi huo.
Hata hivyo Dully alikuwa na msanii mwenzake ‘Tunda Man’ ambaye naye
alipanda jukwaani na kuwasalimu wapenzi wa miondoko hiyo ya kizazi kipya
kwa kuimba mashairi kadhaa ya nyimbo zake.
No comments:
Post a Comment