Pages

Saturday, March 15, 2014

HAYA NDIO MAHUSIANO YA MASTAA WA KIBONGO YALIYOACHA GUMZO KUBWA KWA MASHABIKI BAADA YA KUACHANA.


Kati ya break-up zilizowahi kumake headlines namba moja ni hii hapa,sababu hadi ilikuwa ukimuuliza mtoto mdogo anaweza kukuambia,Sintah akiwa ni muigizaji maarufu sana hapa Town,wakati Juma nature ndio mkali wa Bongo Fleva waliweza ku-date kwa kipindi kirefu kidogo na hii ndio ilikuwa celebrity couple maarufu,ilikuja kufikia Tamati ya penzi lao kutokana na kile kinachosemekana kuwa ni kutoaminiana kwa wawili hawa,hadi kufikia wakati Juma Nature kumuimbia mpenzi wake wimbo uliokuwa unahusu kuvunjika kwa mahusiano yao.
Wema Sepetu & Chaz Baba.


Wakati ambapo jina la Wema Sepetu halikuwa kubwa kama ilivyo hivi sasa,kipindi hicho kabla hata ya story za Diamond hazijawa talk of the town wapenzi hawa wawili walikuwa ndio wako katika mapenzi motomoto,Chaz Baba akiwa ni msanii Mwimbaji maarufu wa bendi,huku Wema Sepetu ndio alikuwa Miss Tanzania mwaka 2006.

Haikujulikana ni nini haswa chanzo cha break-up yao,ila baada tu ya Chaz Baba kuachwa huku bado akiwa anampenda Wema,Wema Sepetu ndipo alikuwa amesha anguka katika Penzi Jipya kabisa la Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz. 

Diamond Platnumz & Wema Sepetu.






Kwa mujibu wa Wema Sepetu mwenyewe,inasemekana kuwa breakup hii ilisababishwa na Jokate,sababu muda walipokuwa wapenzi na mambo yao yalikuwa yanaenda vizuri tu,na hawakuwa na ugomvi wowote uliokuwa unaendelea kati yao,ila mbali na rumors alizokuwa anasikia za hapa na pale na kutoziamini,siku ikafika ndipo alipowakuta wawili hao wakiwa pamoja.


Wema na Diamond mbali na kuwa wameweza kuachana mara nyingi katika kipindi chao cha mahusiano,inaonekana wawili hao wanamapenzi ya kweli,sababu baada ya muda kupita huku kila moja akiwa anakula vyakwake,mwisho wa siku walichoka ku-pretend na kuweza kurudiana hadi hivi sasa penzi lao likiwa bado lipo moto moto.  

Jokate & Diamond Platnumz.


Hii ni moja ya couple iliyowahi kudumu kwa muda mfupi kweli hapa town,ila rumors has it kuwa wawili hawa walikuwa wana-date kisiri sana,haikujulikana kwa hukika walikuwa wapenzi kwa muda gani ila kipindi Diamond Platnumz wana misunderstanding na Wema ndipo Jokate alipoingia kati na kuweza kuchukua nafasi lakini wakati huo huo bado Diamond alikuwa bado yupo Officialy na Wema.Baada ya Wema Sepetu kuwakuta live Diamond na Jokate ndipo inasemekana huo ulikuwa mwisho wa mahusiano yao.  

Hasheem Thabit &Jokate.

Hasheem Thabit akiwa ni mchezaji wa kikapu wa kulipwa huko marekani kutoka hapa Tzee, nae ali-fall katika penzi na Jokate Mwegelo,ingawa mahusiano yao yalikuwa si ya public sana,labda kutokana na Hasheem Thabit kuhamisha makazi yake huko nchini marekani wakati Jokate alikuwa hapa Tanzania,ilikuwa vigumu sana kuwakuta wawili hawa mara kwa mara.

Baada ya muda kupita habari za hapa town zilikuwa ni kwamba Jokate na Hasheem Thabit wali break-up,alipoulizwa moja kwa moja Jokate aliweza ku-confirm habari hizo na sababu za break-up hiyo zilikuwa zinasemekana kuwa ni umbali kati ya wawili hao,huku kila mmoja kutomwamini mwenzake,ila rumors has it kuwa ni kwa sababu Jokate alikuwa anatoka na Diamond. 

Diamond Platnumz & DVJ Penny.


Baada ya Diamond kuachana na Wema,Diamond aliangua kwenye penzi la Dvj maaruf hapa Town,Dvj Penny,mapenzi yao yaliweza kudumu kwa miezi kadhaa,wawili hawa walionekana wamefall kabisa moja kwa moja,waliiva sana katika kipindi chao cha mahusiano hadi pale Diamond alipoamua kurudi kiroho safi tu, kwa mpenzi wake wa Zamani Wema Sepetu.

No comments:

Post a Comment