skip to main |
skip to sidebar
CHUO CHA USAFIRISHAJI KUADHIMISHA VIPAJI KWA TAMASHA LA BURUDANI
CHUO
cha Usafirishaji kilichopo jijini Dar es Salaam, kinatarajiwa
kuadhimisha siku ya vipaji chuoni hapo ambapo mambo mbalimbali
yatafanyika kusindikiza siku hiyo maalum chuoni hapo. Baadhi ya matukio
yatakayofanyika ni pamoja na michezo kama soka, netiboli na kuvuta
kamba. Vile vile burudani mbalimbali kama fashion show, muziki na
vikundi vya kudansi vitakuwepo.
Tamasha hilo litakuwa na matukio mchanganyiko ya kielimu, michezo na
burudani ambapo katika taaluma kutakuwa na hotuba za uhamasishaji,
utengenezaji wa filamu na mengineyo. Kwa upande wa michezo kutakuwa na
mechi za soka ambapo Kitengo cha Manunuzi (Procurement) kitapambana na
Kitengo cha Usafirishaji (Logistics)
Tamasha hilo pia litahusisha uchangiaji wa damu kupitia mradi wa ‘Damu Salama’
No comments:
Post a Comment