Pages

Thursday, July 31, 2014

PICHA 15: HATIMAYE HALI YA BAHATI BUKUKU YAENDELEA VIZURI..SHUHUDIA MWENYEWE HAPA....!




Bahati Bukuku akiwa amekaa nyumbani kwake
Hali ya mwimbaji wa nyimbo za injili Bahati Bukuku inazidi kuimarika na kuendelea vizuri kama chanzo ilivyomshuhudia akiwa nyumbani kwake Tabata, akiwa mwenye furaha kuwaona watu mbalimbali wakiwemo waimbaji wenzake ambao wameenda kumjulia hali.
Bukuku ambaye kwa sasa anaendelea kuutibu mgongo ambao umepata maumivu na wala haujavunjika kama taarifa nyingine zilivyosambazwa.. Pia chanzo ilimshuhudia akiwa amekaa na marafiki zake huku akiendelea kumshukuru Mungu aliyewaepusha na ajali hiyo.

Bukuku anasema kama sio Mungu kuingilia kati basi sasa hivi ingekuwa habari nyingine, kwani mara baada ya lori kuwagonga alijaribu kutoka katika gari alilokuwemo lakini alishangaa anashindwa kuamka ndipo alipogundua kuwa ameumia mgongo lkn kwa sasa hali yake inaendelea vyema. Pia dereva wa gari hilo Edson Mwakabungu ambaye aliumia mguu anaendelea vizuri pamoja na kijana Frank ambaye alipata jeraha dogo kichwani naye anaendelea vyema.

Zifuatazo ni picha zikimuonyesha Bahati Bukuku akiwa na ndugu na marafiki mbalimbali waliofika nyumbani kwake kumjulia hali.

Jennifer Mgendi akizungumza na Bahati
Ambwene Mwasonge akimjulia hali
Gospel Kitaa (GK) ikijadili jambo na Bahati
Irene Mwamfupe (kushoto) pamoja na Ikupa Njela (kulia) wakiwa pamoja na rafiki yao Bahati
Edson Mwakabungu ambaye alikuwa dereva na kuumia mguu katika ajali hiyo akiwapasha kilichojiri marafiki zake
Edson Mwasambwite (kulia) akiwa na Aliko nao walifika kumjulia hali
Ambwene Mwasongwe akisalimia ndugu mbalimbali waliofika
Emanuel Mgogo (mwenye shati jekundu) aliyeimba wimbo unaoitwa Msikilize Mungu akizungumza na Edson

MAOMBI YAKAMIMINWA

No comments:

Post a Comment