Pages

Saturday, August 9, 2014

PICHA ZAIDI YA 52 MWANZO MWISHO KWENYE SHOW YA MATUMAINI JANA , AKIWEMO SHILOLE, ROMA, YEMI ALADE NA WASNII WENGINE KIBAO WAFUNIKA

Mwanadada mwigizaji na mwanamuziki Zuwena Mohamed 'Shilole' akicheza kwa kujiachia katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014 usiku wa kuamkia leo.

Zuwena Mohamed 'Shilole' akiongea na mashabiki wake.
 


Wacheza show wa msanii wa Shishi Baby wakifanya yao.




Shishi Baby akifanya makamuzi.


Shishi Baby akiagana na Mashabiki wake baada ya kufanya makamuzi ya ukweli katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014 usiku wa kuamkia leo.


Roma Mkatoliki akiwarusha vilivyo wapenzi wa burudani waliofurika katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014 usiku wa kuamkia leo.
Roma Mkatoliki akiongea na mashabiki wake.
Mashabiki wakiendelea kucheza na Roma.
Roma Mkatoliki akiendelea kufanya makamuzi.


Staa kutoka nchini Nigeria, Yemi Alade akipiga shoo usiku huu katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014 ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.



Staa kutoka nchini Nigeria, Yemi Alade akipiga shoo katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014 ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Makamu wa Rais Mh. Mohamed Gharib Bilali akisalimiana Makamu wa rais Mh.Mohamed Gharib Bilali akisalimiana na Miongoni mwa matukio yaliyosisimua kwenye tamasha hilo ni pale mechi za mpira wa miguu zilipokuwa zikichukua nafasi.

Yemi Alade akipiga shoo.
BONGO MOVIES VS BONGO FLEVA
Wakati mechi hiyo ilipokuwa ikikaribia kuanza, umati ulilipuka kwa shangwe baada ya kumuona Mfalme wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba alipokuwa alipoonekana akipasha misuli na wenzake.

Mwanamuziki H-Baba akijaribu kuwatoka wachezaji wa Bongo Movies.
Wengi walikuwa wakishangilia wakidai ni siku nyingi hawajamuoana uwanjani, huku wengine wakishangilia kwa kuimba wimbo wake mpya wa Mwana.
Mchezaji wa Bongo Fleva, Ali Kiba akimtoka msanii wa Bongo Movies, Issa Mussa 'Cloud 112'.
Kama hiyo haitoshi haitoshi, shangwe zaidi liliongezeka baada ya Kiba kufunga bao ambalo lilidumu hadi mwisho wa mchezo na kuwafanya Bongo Fleva waibuke kidedea kwa mara nyingine hivi kumfanya kuwa nyota kwenye tamasha hilo.
Nyomi iliyokusanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar kwa ajili ya Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014.
BONGO MOVIES WACHEZA KIDUKU
Licha ya kufungwa, mashabiki wa Bongo Movies ndiyo walionesha kushangilia zaidi ya mashabiki wa Bongo Fleva ambao ndiyo walikuwa washindi.

Wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014.
Walicheza staili ya kiduku ile mbaya huku wakishangiliwa na umati uliofurika uwanjani hapo.
Bondia Mada Maugo amemshushia kichapo bondia Thomas Mashali katika mpambano wao kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini 2014 ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.
WABUNGE SIMBA VS YANGA
Wakati wa mechi ya wabunge, vituko ndiyo ilikuwa balaa. Kuna wakati baadhi ya waheshimiwa wabunge walikuwa wamechoka kiasi cha kushindwa kusogea lakini mwisho wa siku ilikuwa ni burudani kwani waliweza kubadilishana, wengine wakachukua nafasi. Hadi mtanange unamalizika, wabunge wa Yanga waliibuka kidededea kwa ushindi wa mabao 3 kwa 2.

Yanga wakishangilia bao lao.
Matukio mengine yaliyosisimua siku hiyo ni kama wasanii wa Bongo Fleva, Juma Nature, Shilole na wengineo ambao walipanda stejini kwa nyakati tofauti na kutoa burudani baab’kubwa.
Tamasha la Usiku wa Matumaini mwaka huu lilikuwa noma sana!

Ridhiwan Kikwete akishangilia ushindi wa Yanga dhidi ya Simba.

No comments:

Post a Comment