MAJANGA! Msanii wa Hip Hop anayetokea Ilala, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ amedaiwa kumpa kipigo kizito mpenzi wake wa zamani aliyefahamika kwa jina la Mwanaisha Kiboye.
Rashid Makwiro ‘Chid Benz’.
Tukio
hilo lililokusanya umati wa watu lilijiri Jumapili iliyopita maeneo ya
Buguruni (kwenye mafleti) jijini Dar ambapo Chid alikuwa kwenye
mizunguko yake na mpenzi wake wa sasa ambaye jina lake halikuweza
kupatikana mara moja.Kwa mujibu wa chanzo chetu, Chid na mpenzi wake huyo walifika katika baa moja maarufu iliyopo katika mafleti hayo na kumkuta Mwanaisha akiwa amekaa na rafiki zake. Demu huyo alimsalimia Chid na ndipo mtiti ukaibuka.
“Mwanaisha alipomuona Chid anakatiza na kwa kuwa aliwahi kuwa mpenzi wake, akaona siyo ishu bora ampe hai kwa mbali ndipo Chid alipomaindi na kumfuata huku akisema: unajifanya unanijua sana siyo? Ngoja nikuoneshe,” kilisema chanzo.
AMZIMISHA
Chanzo hicho kilizidi kudai kuwa, baada ya Chid kusema hivyo alimshushia kipondo kikali hasa sehemu za usoni na kumsababisha Mwanaisha achanike mdomoni kabla ya kuzimia palepale na kuanza kupepewa na marafiki zake, Chid akatokomea kusikojulikana.
Imeelezwa kuwa, Mwanaisha alipozinduka baada ya kupepewa alikwenda kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Pangani, Ilala ambapo alipewa Fomu ya Polisi Nambari 3 (PF3) kisha kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu, Ilala - Amana.
CHID NAYE AKIMBILIA POLISI
Chanzo kimezidi kueleza kuwa, wakati Mwanaisha akianza kupewa matibabu hospitalini, Chid naye alishauriwa na marafiki zake kwenda kutoa taarifa katika kituo hicho cha polisi kama njia ya kujihami pasipo kujua kuwa ameshawahiwa.
“Marafiki zake walioshuhudia tukio hilo walimshauri jamaa (Chid) akafungue mashitaka polisi kama njia ya kujihami, akakubali ndipo alipokwenda kutiwa nguvuni kwani tayari Mwanaisha alikuwa ameshamuwahi,” kilisema chanzo hicho.
ATUPWA MAHABUSU
Habari zimeeleza kuwa, Chid alipofika kituoni kwa ajili ya kutoa taarifa, alidakwa na kusokomezwa mahabusu kwa vile tayari alikuwa ameshafunguliwa mashitaka.
Chanzo kilichopo polisi hapo kimeliambia Amani kuwa, jamaa alipoambiwa avue mkanda ili atupwe sero alileta ubishi hivyo kusababisha polisi watumie nguvu ya ziada kumdhibiti kwa sababu alisema yeye ni mtu maarufu hivyo hawawezi kumtisha.
AKUTWA NA BANGI
Wakati msanii huyo anayesifika kwa sauti nzito akitaka kuingizwa ndani, alisachiwa na kukutwa na misokoto miwili ya bangi hivyo kuandikishwa kesi nyingine ya madawa ya kulevya mbali na ile ya awali ya kujeruhi.
MWANAISHA ANASEMAJE?
Juzi Jumanne, Amani lililimsaka Mwanaisha ambapo lilifanikiwa kumkuta nyumbani kwao, maeneo ya Sharifu Shamba, Ilala akiwa hawezi kutembea, kuongea vizuri akiwa hoi kitandani.
Akizungumza kwa shidashida, Mwanaisha alisema anasikitika kuona Chid amempiga bila kisa.
“Sijui hata kwa nini aliamua kunipiga, amenipiga vibaya, nimeshonwa nyuzi 12 na bado nasikia maumivu makali kichwani,” alisema.
Kwa mujibu wa dada wa Mwanaisha ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini, watafuatilia kwa karibu mwenendo wa kesi hiyo ili kuona mwisho wake kwani mbali na kumweka majeraha ndugu yake lakini bado hali ni mbaya na wanatakiwa kumfanyia Kipimo cha CT Scan.
“Hizi gharama zote tutakazohangaika kumtibu ndugu yetu lazima Chid azilipe maana amempiga ndugu yetu pasipo kufanya kosa lolote,” alisema dada wa Mwanaisha.
APANDISHWA KIZIMBANI
Kwa kuwa Jumapili na Jumatatu ilikuwa Sikukuu ya Pasaka, juzi Jumanne Chid alipandishwa katika Mahakama ya Mwanzo - Ilala na kusomewa mashitaka mawili; KUJERUHI na KUKUTWA NA BANGI.
Siku hiyo, mahakama ilimsomea mashitaka na kutakiwa kujibu kama ni kweli amefanya makosa hayo lakini mshitakiwa huyo alikanusha makosa yote mawili hivyo kesi hizo kuahirishwa.
KESI ZATOFAUTISHWA
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika mahakama hiyo, kesi ya kujeruhi inatarajiwa kutajwa tena mahakamani hapo Aprili 24, mwaka huu (leo) huku ile ya kukutwa na bangi ikisogezwa mbele hadi Mei 6, mwaka huu.
APATA DHAMANA
Baada ya kuahirishwa kwa kesi hizo, mshitakiwa alipewa nafasi ya kupata dhamana kwa masharti ya kulipia shilingi 100,000 huku akidhaminiwa na watu wawili ambapo Chid alitimiza masharti hayo na kuachiwa huru kusubiri kesi zitajwe tena.
Kamanda wa Mkoa wa Polisi Ilala, ACP Marieta Minangi amekiri kutokea kwa tukio hii,CHANZO GPL
No comments:
Post a Comment