Msanii
chipukizi wa muziki wa kizazi kipya Msomi John a.k.a War killer
akiwapagawisha wakazi wa jiji la Dar es Salaam katika Tamasha la Cheka
Bombastik lililoandaliwa na Vodacom Tanzania mahususi kwa ajili ya
wateja wake katika msimu huu wa sikukuu ya pasaka na kufanyika kwa siku
mbili mfululizo katika fukwe za bahari ya hindi coco beach.
Mwanaidi
Jumanne akiwa kwenye Swagga la ukweli la pasaka katika Tamasha la Cheka
Bombastik lililoandaliwa na Vodacom Tanzania mahususi kwa ajili ya
wateja wake katika msimu huu wa sikukuu ya pasaka na kufanyika kwa siku
mbili mfululizo katika fukwe za bahari ya hindi.
Msanii
chipukizi wa muziki wa kizazi kipya Amir Jabir mkazi wa Namanga jijini
Dar es Salaam akiwapagawisha wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwenye
Tamasha la Cheka Bombastik lililoandaliwa na Vodacom Tanzania mahususi
kwa ajili ya wateja wake katika msimu huu wa sikukuu ya pasaka na
kufanyika kwa siku mbili mfululizo katika fukwe za bahari ya hindi.
Msanii
mahiri wa muziki wa kizazi kipya wa kundi la TMK Family Chege
akiwapagawisha wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwenye Tamasha la Cheka
Bombastik lililoandaliwa na Vodacom Tanzania mahususi kwa ajili ya
wateja wake katika msimu huu wa sikukuu ya pasaka na kufanyika kwa siku
mbili mfululizo katika fukwe za bahari ya hindi coco beach.
Nyomi
ya watu iliyofurika kwenye Tamasha la Cheka Bombastik lililoandaliwa na
Vodacom Tanzania mahususi kwa ajili ya wateja wake katika msimu huu wa
sikukuu ya pasaka na kufanyika kwa siku mbili mfululizo katika fukwe za
bahari ya hindi jijini Dar es Salaam.
Dar
es Salaam, Katika kusheherekea sikuu ya Pasaka, wasanii Chege Chigunda
au mtoto wa Mama Saidi na mwenzake YP wametoa burudani ya aina yake kwa
wakazi wa Dar es Salaam katika tamasha maalum la Cheka Bombastik
lililofanyika katika fukwe za Coco jijini Dar es Salaam.
Burudani
ilianza kwa staili ya aina yake kwa wasanii Chipukizi “Underground”
kupanda jukwaani na kutoa burudani kwa maelfu ya mashabiki waliojitokeza
katika fukwe hizo.
Uwanja
ulikuwa hautoshi pale alipopanda jukwaani Chege Chigunda na kuwapeleka
Mashabiki wake Uswazi Take Away, kwa kuifanya kazi yake vyema na kutoa
burudani ya Kipekee kwa pamoja waliimba nyimbo kadhaa za kundi la
Wanaume Family.
Akizungumza
na waandishi wa habari punde baada ya kumalizika kwa Tamasha hilo,
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, ambao ndio waandaaji wa
Tamasha hilo, Matina Nkurlu amesema kuwa Imekuwa kawaida kwa kampuni yao
kutoa burudani kwa Wakazi wa Dar es Salaam na Sehemu nyingine katika
ziku za siku kuu.
“Umekuwa
ni Utaratibu wetu wa kawaida wa kutoa burudani kwa Watanzania ambao
wamekuwa wakituunga mkono siku zote na kutufanya kuwa namba moja kila
siku,” alisema Nkurlu na kuongeza, Umati huu ni ishara tosha ya namna
wakazi wa Dar es Salaam walivyo kubali burudani hii”
“Burudani
hii ni Maalum kwa wale wote ambao wanapenda kupumzika katika sehemu za
Fukwe kama Coco Beach, tunatambua kuwa kipindi hiki wengi wanapenda
kupumzika na familia zao hivyo ni vyema pia wakapata burudani ya aina
hii.” Alisema Nkurlu.
Meneja
huyo alisema kuwa burudani hiyo ni ya siku mbili, siku ya tarehe 20 na
21 ya Mwezi April ambayo ni jumapili na jumatatu ya pasaka, na wateja wa
Vodacom watakao jitokeza katika Tamasha hilo, watapata zawadi
mbalimbali na wataunganishwa na huduma ya Cheka Bombastik Bure, Ili
kuweza kupiga simu kwa bei nafuu.
“Tumefanya
Tamasha hili tukiwa na ujumbe maalum kwa wateja wetu wa Vodacom
kuhakikisha wanajiunga na huduma yetu ya Cheka Bombastik ambayo inawapa
nafasi ya kuchagua bando za aina mbali mbali za kupiga simu, Vodacom
kwenda Vodacom au kutoka Vodacom kwenda mitandao mingine.” Alihitimisha
Nkurlu.
No comments:
Post a Comment