Pages

Thursday, June 12, 2014

VANESSA MDEE KUZINDUA VIDEO YAKE YA COME OVER JUMAMOSI HII


Vanessa Mdee anatarajia kuzindua video ya wimbo wake ‘Come Over’ Jumamosi hii ya June 14. Akiongea na Mtandao huu, Vanessa aka Vee Money  amesema hakuwahi kusema chochote kuhusu kushoot video hiyo kwakuwa anapenda kuwasurprise mashabiki wake.
“Napenda nifanye kitu ambacho watu hawategemei ndio maana hata nilipoenda kushoot video kulikuwa hakuna picha, kulikuwa hakuna behind the scenes, kulikuwa hakuna clips, kulikuwa hakuna Instagram post. Kila mtu ambaye alikuwa onset aliambiwa ‘no one is allowed to tweet, no one is allowed to instagram,” amesema.
Vanessa ameongeza kuwa video ya Come Over imefanywa na director wa Kenya aliyeongoza video ya Weusi ya wimbo wao Gere na ile ya Sauti Sol, Nishike.

Pamoja na video hiyo mshindi huyo wa wimbo bora wa rnb wa tuzo za Kili, anatarajia kuachia wimbo mpya uitwao ‘Hawajui’ uliotayarishwa na Nahreel.

No comments:

Post a Comment