Pages

Monday, March 10, 2014

SOMA ALICHOKISEMA NASH MC BAADA YA WIMBO WAKE WA [ KAKA SUMA ] KUFUNGIWA TCRA

TAARIFA KWA UMMA: Siku ya trh 7 - 3 - 2014 mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA imetoa onyo kwa kituo cha radio (RFA) baada ya kuwa wamecheza wimbo wangu uitwao "KAKA SUMA" wakidai ni kinyume cha sheria za utangazaji na kwamba kufanya hivyo ni "UCHOCHEZI" uliofanywa na radio hiyo.Binafsi naendelea kusikitishwa na mambo mengi hapa nchini likiwemo na hili la TCRA.Wimbo huo uliotoka mwaka jana kati ya mwezi wa 6 na wa 7 ulichezwa ktk vituo mbali mbali vya radio nchini na umefikish...a ujumbe kwa 100% pasi na shaka,Kuendelea kutujengea hofu kwa kusema ukweli ndio chanzo cha uvunjifu wa amani.Ikumbukwe kuwa kila mtu ana uhuru wa kutoa na kupokea habari bila ya kuingiliwa kwa mujibu wa katiba ya sasa na ndio maana vyombo vya habari vinanyimwa uhuru kwa mchakato wa sasa wa kuelekea kupata katiba mpya.Nawakumbusha,hii ni sanaa na ndio kazi kubwa ya "HIP HOP" na ndio njia sahihi ya kufikisha ujumbe kwa jamii sasa nashangazwa na sentesi ya uvunjifu wa amani.Ukweli siku zote una nguvu na unapingwa vikali.Yanayoendelea bungeni ni udumishaji wa amani? Mafisadi wanaokamatwa ni udumishaji wa amani?? Mauwaji ya Tembo na biashara za dawa za kulevya zinazohusisha vigogo ni udumishaji wa amani? Je ni kweli hakuna nyimbo zinazochochea mambo maovu na mabaya nchini zaidi ya KAKA SUMA? Bora kufa umesimama kuliko kuishi kwa kupiga magoti.Nasubiri kusikia tena wimbo wa Nash Mc uitwao "NAANDIKA" ukifungiwa pia.

No comments:

Post a Comment